Welcome to this forum where we share knowledge about a number of issues related to people's livelihoods. Karibu katika ulingo huu tubadilishane mawazo juu ya maisha ya watu.
Saturday, September 24, 2011
Thursday, September 22, 2011
Mazimio 14 juu ya Hatma ya Ardhi na Mchakato wa Katiba Mpya Tanzania
Mazimio 14 juu ya Hatma ya Ardhi Tanzania na Mchakato wa Katiba Mpya.
Ni siku ya nne na ya mwisho la Kongamano la 10 la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia eneo la Mabibo Jijini Dar es salaam. Kongamano limeandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) likishirikiana na Mashirika yanayotetea Haki za wanawake, haki za binandamu, rasilimali na makundi maalum (FemAct) na kuhudhuiwa na washiriki zaidi 3,500 kutoka pande zote za Tanzania yaani Bara na Visiwani. Mada kuu ikiwa ni Jinsia, Democrasia na Maendeleo: Ardhi, Nguvu Kazi na maisha endelevu.
Katika Kongamano hili mada kuu iligawanywa katika warsha Nane, Warsha namba moja ikiwa ni Mapambano katika usimamizi na matumizi ya maliasili katika muktadha wa ‘Uporaji wa Ardhi’ na washa ya pili ni Mapambano kuhusu upatikanaji wa katiba zenye maslahi ya wananchi Afrika, tatu ilihuusu Jinsia na Utu:Siasa za Chaguo na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kazini – sekta rasmi na zisizo rasmi, Nne ni Siasa za biashara, misaada na madeni, tano ni Hakia ya huduma Bora inayozingatia mahitaji ya kijinsia: Elimu, Sita ilijadili Haki ya huduma bora inayozingatia mahitaji ya kijinsia: Afya ya Uzazi, warsha ya saba ilijikita katika Mapambano ya kupata Uongozi wezeshaji, Demokrasia na Siasa shirikishi:wanawake na Ushiriki kwenye Siasa, na Warsha namba Nane ililenga zaidi Haki ya huduma Bora inayozingatia mahitaji ya kijinsia:Maji na Nishati.
Warsha zote zilijadiliwa kwa siku zote nne na washiriki waliweza kugawanyika kulingana na maeneo yao na muktadha mzima wa kongamano. Lengo la mgawanyiko wa warsha ni kuwawezesha washiriki waweze kushiriki kikamilifu katika maeneo wanayoyapenda ili mwisho wa Kongamano waweze kuwa na tamko la pamoja juu ya nini wanaazimia kufanya na namna ya kutekeleza.
Katika Warsha namba moja na ambayo makala haya inachambua zaidi ni mada kuu ikiwa ni Mapambano katika usimamizi na matumizi ya maliasili katika muktadha wa ‘Uporaji wa Ardhi’. Taasisi ya HAKIARDHI ilipewa jukumu la kuratibu warsha hiyo kwa siku zote za Kongamano. Warsha hii pamoja na kuwa ilibeba muktadha mzima wa Kongamano iliweza kuibuwa masuala mbalimbali ya Ardhi kuanzia utawala wa ardhi, uwekezaji na hofu ya wananchi wengi juu ya uwepo wa sheria za ardhi za sasa kuonekana kutomlinda zaidi mwananchi wa kawaida na mwishoe washiriki waliazimia kwa pamoja juu ya mambo mbalimbali ya kuzingatiwa ili kuweza kuwa na katika mpya inayojali haki sawa katika kupata na kutumia raisilimali ardhi.
Suala la utawala wa ardhi lilijadiliwa kwa mapana zaidi na washiriki kuibuwa mambo mbalimabli ambazo ni kikwazo kabisa katika utawala wa ardhi. Mjadala ulianza baada ya uwasilishwaji uliofanywa na Afisa Ardhi Mteule Bi Grace kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyezungumzia swala la ardhi kwa mapana zaidi ambapo kwa upande wake alibainisha kuwa sheria za ardhi zilizopo ni nzuri na zinalinda haki za wenyeji japo utekelezaji unakuwa vinginevyo kutokana watendaji wabovu na rushwa iliyo kithiri.
Akichangia katika mada Bi. Mercelina kutoka Morogoro alibainisha kuwa tatizo ni mahakama zetu zinazo shughulikia keshi za Ardhi kwani kesi huchukuwa muda mrefu na uwezo wa mkulima mdogo au mfugaji kupata haki ni ngumu sana na wenye uwezo (wawekezaji) ndio wanaoshinda na sio kwasababu wanahaki bali kwasababu wanapesa.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Arash kutoka Loliondo Ngorogoro Bwana Kyaro Ormins alibainisha kuwa tatizo ni uroho wa baadhi ya viongozi wa serikali kupenda fedha kuliko watanzania wanaowatumikia huku akitoa mfano wa uwepo wa mwekezaji wa Ortello Bussines Corperation(OBC) kutoka Falme za Kiarabu anayependelewa zaidi Loliondo kuliko wananchi wenyeji. Pia mwenyekiti huyo aliweka wazi pia mchakato wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ulioandaliwa kutoka Wizara ya Ardhi bila kuwashirikisha wananchi wa eneo hilo kama inavyo tamkwa katika sheria ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi namba 6 ya mwaka 2007 juu ya ushiriki kamilifu wa wananchi na wadau wote katika mchakato.
Bi. Anna Oloshiro kutoka Kilosa Morogoro alibainisha pia kuwa sheria za Ardhi sio nzuri kwani Rais amepewa mamlaka makubwa katika ardhi kuwa yeye ndiye mwenye Milki ya Hatma juu ya Ardhi na hii hutumika sana kuwanyang’anya ardhi watu wenye kipato duni. Umilki wa Hatma aliopewa Rais na matumizi ya neno ‘Manufaa ya Umma’ imewaathiri sana wafugaji.Je umma ni nini?kama sio kisingizio cha upokonyaji wa Ardhi kama inavyowatokea wafugaji kuhamishwa hamishwa? Alihoji Anna Oloshiro.
Baada ya mjadala uliochukuwa siku mbili mfululizo ilifika siku ya tatu ambapo wana warsha na Kongamano wote wanatakiwa kuwa na maazimio ya nini kifanyika na namna gani kifanyike na nani atahusika.
Kwa upande wa Warsha ya Ardhi juu ya Mapambano katika usimamizi na matumizi ya maliasili katika muktadha wa ‘Uporaji wa Ardhi’ ambapo iliratibiwa na HAKIARDHI wana warsha waliazimia mambo 14 ambayo ni ya msingi kabisa UMMA wa Watanzania kupitia vyombo vya habari unapaswa kujuwa ili hatua ziweze kuchukuliwa. Mazimio hayo yalisomwa mbele ya Washiriki wa Kongamano na Godfrey Massay (Afisa Programu) kutoka HAKIARDHI. Mazimio hayo ni: Kwanza Ardhi liwe suala la Kikatiba na Katiba mpya ieleze bayana juu ya Mamlaka katika Ardhi na maamuzi yatakayofanyika yawe yanazingatia utaratibu utakao tambuliwa na Katiba.
Pili, masuala ya wananchi yapewe kipaumbele katika uwekezaji kwenye Adhi. Hili lilijitokeza mara kwa mara kutokana hali halisi ya uwekezaji katika nchi yetu ya wawekezaji kupewa kipaumbele kuliko wenyeji.
Tatu, Serikali iwashiikishe wananchi katika utungaji wa sera na sheria zinazohusu usimamizi wa rasilimali. Nne, Serikali iwe na mkakati dhabiti na sawia katika utoaji wa elimu kwa umma juu ya masuala mbalimabali ya upatikanaji, utumiaji na umiliki wa rasilimali.
Tano, Vyomba vya usimamizi wa ardhi kuanzia ngazi ya kijiji, wilaya, hadi taifa vizingatie zaidi sheria na kanuni katika utekelezaji. Sita, Asasi za Kiraia ziimarishe na kuendeleza elimu ya Haki za Ardhi kuanzia ngazi Kijiji. Saba, Kuwa na mkakati dhabiti na utekelezaji wa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi na hasa uwashirikishe wanachi wa maeneo husika (participatory approach) na sio mfumo wa kutoka Wizarani kwenda kijijini (Top down uproach). Tisa, Wazalishaji wadogowadogo wawe muhimili mkubwa katika mapinduzi ya Kijani (Kilimo Kwanza). Kumi, Wanawake waungane katika kudai haki zao kupinga unyanyasaji. Kumi na moja, serikali ichukuwe jukumu la kuwaajibisha watendaji wanao enda kinyume na sheria badala ya kuwaacha waendelee kuboronga. Kumi na mbili, Mahakama na Mabaraza ya ardhi zizingatie zaidi sheria na uhalisia pamoja na kutoa maamuzi ya haki na za wakati badala ya kuangalia maslahi ya wenye pesa zaidi.
Kumi na tatu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoe tamko juu ya mgogoro wa Loliondo. Suala la loliondo limekuwepo kwa muda mrefu sana na tume nyingi zimeanzishwa bila kuwa na mrejesho wowote kwa wananchi.
Pamoja na maazimio hayo yaliyosomwa mbele ya washiriki wa Kongamano pia lilitolewa suala la maandamano nchi nzima pale ambapo masuala magumu ya ardhi yasipotolewa maamuzi na serikali basi wananchi na wanaharakati kwa ujumla waandamane kudai usuwa katika rasilimali.
Imeandaliwa
Na; Valentin Ngorisa

Subscribe to:
Posts (Atom)